Friday, June 20, 2014
haya ndo yaliyowakuta uganda baada ya kupinga ushoga
Marekani imeadhidhibu Uganda kwa kuweka
sheria kali ya kupinga mapenzi ya jinsi moja
katika taifa hilo.
Msemaji wa Whitehouse, Caltlin Hayden
ameeleza katika barua yake kwa vyombo vya
habari kuwa sheria iliyopitishwa na bunge la
Uganda ikiuka haki za binadamu.
Vikwazo vya Marekani kwa Uganda kama
adhabu, vinajumisha kuwapiga marufuku
wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo
kutoingia Marekani.
Marekani itapunguza ushirikiano na Wizara ya
Polisi na Afya za Uganda, na kuachana na
mpango wa mazoezi ya kijeshi kati ya
wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa
Uganda.
Uganda walipitisha sheria ambayo inaeleza
wazi mtu atakayekutwa na hatia ya kushiriki
katika masuala ya ushoga atahukumiwa
kifungo cha maisha jela.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment