Saturday, June 21, 2014
Msami akili kuwa mpenzi wa iren uwoya
Mkali wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa
kuvunja (dancer) amezungumzia uhusiano
wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies,
Irene Uwoya.
Akiongea na Times Fm, Msami alizunguka sana
mbuyu kutaka kutoa maelezo kuhusu ukweli
wa mambo kati ya wawili hao lakini kwa mara
ya kwanza aliamua kuiambia Times Fm kauli
yake kutokana na jinsi alivyoulizwa.
“Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach
ili apate jibu. Ni kweli (kicheko)…
nimekuridhisha lakini, nimeamua
kukuridhisha.” Amesema Msami..
Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa
muonekano uliwafanya wengi wazungumze
kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami
amegeuka Serengeti Boy kwa Uwoya ambaye
wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli
ni kwamba Msami ni mkubwa kwa Uwoya.
“Unajua mimi mwanzo, Serengeti Boy nilikuwa
sina tafsiri yake kabisa yaani. Yaani ile deeply
nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Kwa
hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake ‘Serengeti
Boy’ kumbe ni mtu ambaye amezidiwa umri.
Tofauti na mimi nilivyokuwa nawaza kuhusu
Serengeti Boy.
“Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we
are best friends lakini (joke), lakini mbona
mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni
mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri.
Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi
mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi.
Mimi ni mkubwa kwa Uwoya.” Amesema
Msami
Katika hatua nyingine, Msami ameeleza
mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya
pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.
Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye
mhusika mkuu na kwamba ni filamu ambayo
itahusisha dance na muziki.
Filamu hiyo itatoka mwaka huu lakini bado
haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.
“Movie inakuja very soon, watu wakae tayari.”
Amesisitiza.
Credit: Times Fm
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment