Saturday, June 21, 2014
Mchungaji gwajima apasua jipu....Aitisha kikao kizito
Wakati mume wa mwimba Injili Bongo, Flora
Mbasha, Emmanuel Mbasha akiachiwa huru
kwa dhamana kufuatia kesi ya kudaiwa
kumbaka shemejiye, Mchungaji wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam,
Josephat Gwajima ameibuka na kunena mazito
kuhusiana na sakata hilo.
Mbasha aliachiwa kwa dhamana juzi akitokea
Gereza la Keko, Dar baada ya kupandishwa
kizimbani kwa mara ya kwanza katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juni 17, mwaka
huu na kusomewa mashitaka mawili ya ubakaji
ambayo hata hivyo, aliyakana.
ILIVYOKUWA KORTINI
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya
Ilala, mheshimiwa Wilbeforce Luago siku hiyo
ya Juni 17, alitoa hoja kwamba upande wa
jamhuri hauna pingamizi hivyo dhamana ipo
wazi.
Alisema mshitakiwa alitakiwa kuwa na
wadhamini wawili, mfanyakazi wa serikali na
wa kutoka katika taasisi inayotambulika
sanjari na shilingi milioni 5 kila mmoja.
Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo
siku hiyo hadi hadi juzi alipotimiza,
akaachiwa.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo
ambaye ni wakili wa serikali, Nassoro Katuga
bila kuchelewa aliitaja kesi hiyo yenye namba
CC/186/2004 ambapo rafiki wa Mbasha
aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na
baba wa mtuhumiwa aitwaye Mwahimu Juma
ndiyo waliofanikisha dhamana hiyo. Kesi yake
itatajwa tena Julai 17, 2014.
GWAJIMA SASA
Akizungumza na mwanahabari wetu juzi wakati
Mbasha akiwa nje kwa dhamana, Mchungaji
Gwajima alieleza namna ambavyo sakata hilo
limeitikisa Injili nchini Tanzania kutokana na
kuibuka kwa madai mengi likiwemo suala la
Flora kusemekana amehamia nyumbani kwake
kitu ambacho alikipinga.
Gwajima alisema anasikitika sana kuona ndoa
ya Flora na Emmanuel Mbasha inatikisika
akizingatia Flora ni muumini wake hivyo moja
kwa moja ugomvi wao unaonekana kutia
dosari mwenendo mzima wa uinjilishaji katika
jamii.
“Naumizwa sana na sakata hili lakini hivi
karibuni niliamua kuwaita ndugu wa pande
zote mbili (Flora na Mbasha) nikazungumza
nao kwa kirefu na tukamaliza tofauti zote
lakini tatizo likabaki lile la kisheria zaidi
(mashitaka ya ubakaji kwa Emmanuel),”
alisema Gwajima ambaye makao makuu ya
kanisa lake yapo Kawe jijini Dar.
AANDAA TAMKO ZITO
Mchungaji Gwajima alisema kutokana na
sakata hilo kugusa Injili, ameandaa tamko zito
ambalo atalitoa rasmi atakaporudi safari yake
ambayo hakueleza anakokwenda.
“Hatuwezi kukaa kimya juu ya hili, nasafiri
lakini nikirudi tu nitatoa tamko rasmi kwa
kuwaalika waandishi wa habari,” alisema.
IBADANI JUMAPILI
Katika hatua nyingine, ndani ya ibada ya
kanisa hilo iliyofanyika Jumapili iliyopita,
Mchungaji Gwajima alitumia dakika kama 15
katika mahubiri yake kutupa kile kilichodaiwa
kuwa ni jiwe gizani ambapo wengi waliamini ni
kuhusiana na sakata hilo.
“Mimi siyo kama wale, sijibu hoja kama zile,
mfano ukiwa unaoga halafu chizi akachukua
nguo zako na ukamkimbiza nani ataonekana
chizi? Tatizo la Watanzania ni kuwa wakisikia
kitu kipya kinaanza kwao badala ya
kukithamini wanakididimiza ili kisiendelee,
lakini mimi siyo kama wao,” alisema.
Aliongeza: “Mimi kila mwaka naenda Japan na
ninawa-lecture Wajapani ambao pia huja hapa
kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu
watakuja Septemba, lakini Watanzania
hawashtuki na kuja kujifunza juu ya ufufuo wa
wafu wengi wao wanakalia kuandika stori
kwenye magazeti lakini mimi siyo kama wale.”
AMEFUNGUKIA SAKATA LA MBASHA?
Ingawa Mchungaji Gwajima hakueleza moja
kwa moja kuhusu tukio la Mbasha lakini
maneno hayo yalitafsiriwa kwamba ni ya
kujibu hoja zinazomhusisha yeye na tukio hilo.
Anaendelea:”Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53
duniani na nyingi za Ulaya na Marekani halafu
mtu amekaa Magomeni miaka yote
anatengeneza stori ya gazeti, unatarajia
niijibu, mimi siyo kama wale nimetumwa na
nina kazi natakiwa kuifanya duniani na siwezi
kufa mpaka niimalize.”
“Inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla
ya mimi, kwa kuwatungia stori hizo za uongo
lakini mimi siyo kama wale na mwezi huu wa
nane ninaendelea na mkutano Iringa, waache
waandike lakini mimi ni chombo kingine na
siyo kama wale.”
DONGO GIZANI?
Baadhi ya waumini waliokuwa katika ibada
hiyo, walibaki njia panda na katika giza nene
ingawa wengi waliamini alitupa vijembe katika
sakata la Mbasha haswa alipokuwa akisema,
‘mimi siyo kama wale’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment