Saturday, June 21, 2014
Wafahamu wasanii wa Africa watakao preform kwenye tuzo za BET 2014
Tuzo za BET mwaka huu zitatolewa wikend
ijayo, July 28/29 mwaka huu huko Los Angeles
Marekani na kushuhudia wasanii wengi
wakubwa duniani wakiperform kwenye jukwaa
hilo kubwa..
Majina ya wasanii wakubwa wa Afrika
yaliyotajwa ni pamoja na rapper kutoka
Nigeria, Sarkodie, Tiwa Savage wa Nigeria na
kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini ambao
watajumuika na wenzao kuperform Live katika
jukwa hilo, Jumamosi, June 28 huko Los
Angeles.
Hii ni mara ya kwanza kwa wasanii walio
kwenye kipengele cha International acts
kuperform katika tuzo hizo kubwa na zenye
heshima zinazoandaliwa na kituo cha Black
Entertainment Television (BET).
Diamond Platinumz kutoka Tanzania ni
miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo hizo
kwa mwaka huu, na yuko katika kipengele cha
Best International Act akiwa na Mafikizolo,
Tiwa Savage, Davido, Sarkodie na Toofan.
Mchekeshaji Chris Rock na Emmy watakuwa
hosts kwenye tuzo za BET mwaka huu ambazo
zitaangaliwa zaidi na waafrika kulinganisha na
miaka ya nyuma kutokana na ushirikishwaji wa
ziada wa wasanii wa Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment