Sunday, June 29, 2014

Hili ndicho alicho kisema diamomd baada ya tuzo za BET aliyo kuwa akiwania kuchukuliwa na davido

Baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz aliyekua anawania pia tuzo hiyo ameandika ya moyoni kwa watu wake. "Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo. "Katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa. "Cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi kunisupport"


Posted by flavian kachira

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews