RIYAMA Ali mwigizaji wa kike asiye na kashifa katika tasnia ya filamu Bongo, amefunguka kwa kusema kuwa kama kuna msanii mwenzake au mtu mwenye mapenzi naye angependa kama ana sifa kuhusu yeye katika umahiri wa kuigiza na mengineyo basi atumie nafasi hiyo akiwa hai, haitaji kusifiwa akifariki kwani anaamini kuwa sifa hizo hatazisikia. “Nasema mapema kabisa sitaki kusifiwa nikifa, sifa mtu uipate ukiwa hai kama ni faida au kufurahia mwenyewe ujionee lakini nimeshafumba macho kuna faida gani, sisikii sioni haya ya nini kwangu miye?,” anasema Riyama. Msanii huyo amesema kuwa imekuwa tabia kwa baadhi ya wasanii kuleta maigizo katika misiba ya wasanii inapotokea.Mara nyingi waonapo televisheni hujipanga kwa ajili ya kuhojiwa na waandishi na kujifanya kuwa na urafiki na marehemu hata kama walikuwa na ugomvi.
Posted by flavian kachira
No comments:
Post a Comment