Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu walibaki katika nchi hiyo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.
Mugabe aliwaambia wafuasi wa Chama chake katika mkutano wa hadhara kuwa “hatuwataki wakulima wazungu, kumiliki mashamba yetu, lazima waondoke,” Chama cha wakulima wazungu, kimesema kuwa kauli ya Mugabe inasikitisha sana na kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.
Kwa mujibu wa BBC, Wakosoaji wa Rais Mugabe, wanasema kuwa sera yake kutaka kumiliki mashamba yote yanayomilikiwa na wazungu, ndio ilisababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 200-2009
Posted by flavian kachira
No comments:
Post a Comment