Monday, June 23, 2014
mzee majuto: maisha yang ni komedi tosha
Mchekeshaji wa muda mrefu Amri
Athuman 'Mzee Majuto' ametoa kali ya
mwaka baada ya kusema kuwa maisha
yake ni komedi tosha kutokana na
kumvunja mtu mbavu bila kujali yuko
mahala gani....
Akizungumza na mwandishi wetu, Mzee
Majuto alisema yeye hutoa shoo muda
wowote bure bila kujali yuko katika
wakati gani kwani maisha yake ni komedi
tupu...
"Maisha yangu ni komedi tosha,siwezi
kuacha kuchekesha.Wakati mwingine si
kwa kupenda bali huwa najikuta tu
nimefanya hivyo , inabidi watu wanizoee
tu....
"Huwa sina nia ya moja kwa moja
kuchekesha watu, lakini kumbe kauli zangu
huwavunja mbavu.Sijisikii vibaya kwa hilo,
najivunia kuendelea kuwa msanii
ninayekubalika hadi umri huu," alisema
mzee Majuto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment