Wednesday, June 25, 2014
Nando ataganza kuacha kutumia dawa za kulevya (unga)
Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa
‘The Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa
alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa za
kulevya.
Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha
100.5 Times Fm, Nando amesema alikuwa
anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda
mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16
tangu afanye uamuzi wa kuacha.
Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia
dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya
starehe aliyoishi vilichochea.
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu
mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto
kama watu wanavyosema. Na pia pressure na
watu nilokuwa nao wakati ule, na life nililoishi
mimi...ni yale maisha ya kujiachia.” Amesema
Nando.
Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana
na dawa za kulevya (unga) lakini bado
anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza
idadi.
“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia
moja au mbili kwa siku.”
Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu
wenye kibali cha kuvuta bangi kwa maelezo ya
daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la
kuacha kutumia unga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment