Wednesday, July 9, 2014

Sababu ya watengenezaji wa filamu ya Transformers kushitakiwa


Kampuni moja ya kitaliii kutoka nchini China
imesema kuwa itawashtaki watengenezaji wa
filamu mpya ya Transformers kwa kuvunja
mkataba.

Kampuni ya Chongqing Wulong Karst Tourism
Co Ltd imesema katika taarifa yake kuwa
watengenezaji wa filamu hiyo wameshindwa
kuonyesha lebo yao vizuri katika filamu hiyo
kama walivyoahidi.

Wanasema itafungua kesi dhidi ya kampuni ya
Paramount Pictures na moja ya washirika
wake kampuni kutoka China.

Paramount bado haijasema chochote mpaka
sasa kuhusiana na madai hayo

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews