
Mbunge wa viti maaluma Arusha Catherine
Magege ameiomba serikali kuanzisha kanda
maalumu ya kipolisi kwa jiji la Arusha ili
kuimarisha ulinzi ambao umekuwa ukizorota
siku hadi siku huku maisha wa wakazi wake
yakiwa hatarini.
Kufuatia mfululizo wa mabomu baadhi wa kazi
wa jiji la Arusha wameiomba serikali kuingilia
kati swala hilo kwa kuwa watu wamekuwa na
hofu ya kushiriki katika matukio mbalimbali
hasa yale ya mikusanyiko ya watu kwa kuhofia
milipuko.
Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Tanzania
linawashikilia watu wawili kuhusiana na
mlipuko uliotokea katika Mgahawa wa Vama
Traditional Indian Culture uliopo karibu na
viwanja vya Gymkhana na Mahakama Kuu Jijini
Arusha.
No comments:
Post a Comment