Kama ulitazama tuzo za BET 2014 utagundua kuwa ilikuwa ngumu kujua yule binti aliyekuwa na Lil Wayne ni nani sababu ya kubadilika kwake.
Yule binti anaitwa Reginae Carter na ni mtoto wa Rapper Lil Wayne ambaye hivi karibuni ametajwa kuwa msanii mpya kwenye kundi la YMCMB [Young Money Cash Money Brothers ] .
Reginae mwenye miaka 15 sasa alipanda kwenye jukwa wakati Young Money wameitwa kupokea tuzo. Reginae ametoa kazi yake mpya aliyoipa jina “Mind Goin Crazy.
” kutoka kwenye album yake ya kwanza itakayoitwa Becoming Reginae Inayotoka mwaka huu.
Posted by flavian kachira
No comments:
Post a Comment