Friday, July 4, 2014

Mkuu wa chuo na vigogo wengine 7 wa chuo cha uhasibu Arusha watiwa mbaroni

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa
Johannes Monyo na wenzake saba
wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha wakituhumiwa kwa makosa manne
tofauti yakiwemo ya uhujumu uchumi na
kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh
6,258,448.60.
Profesa Monyo na wenzake walisomewa
mashtaka manne tofauti jana mahakamani
hapo na Mwendesha Mashtaka Adam Kilongozi
aliyekuwa pamoja na Hamidu Singano.
Katika shikata la kwanza, Profesa Monyo na
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi chuoni hapo,
Jerome Augustino inadaiwa kuwa Septemba
30, 2011 wakiwa waajiriwa kwa nafasi zao
walizitumia vibaya kwa kubadilisha matumizi
ya vifaa vya umemejua (solar) kwa manufaa
yao binafsi.
Aidha, katika shitaka la pili wanaohusishwa ni
Jerome Agustine, Chacha Wambura, Mpoki
Mwasaga, Papias Njaala, Mathew Melita, Mary
Thomas, Elisaria Kisanga na Gerald Malisa
ambao inadaiwa kuwa, kwa pamoja wakiwa
wajumbe wa bodi ya manunuzi walitumia
nyadhifa zao vibaya na kuidhinisha manunuzi
ya sola hiyo yenye thamani ya Sh
6,258,448.60 kwa kutumia utaratibu wa kuipa
zabuni kampuni ya Helvetic Solar
Contractrors .
Katika shitaka la tatu, watuhumiwa
Augustino ,Faraji Mnyepe na Honory Mkelemi
kwa pamoja inadaiwa kuwa kati ya Novemba 1
na 30 mwaka 2011 katika utekelezaji wa
majukumu yao, kila mmoja waliwezesha
mchakato wa malipo kwa kampuni ya sola ya
Helvetic Solar Contractors kwa kutoa malipo
ya Sh 6, 258,448.60
Na shitaka la nne, Profesa Monyo na
Augustine wanadaiwa kuwa mnamo Juai na
Novemba 30 /2011 wakiwa waajiriwa chuoni
hapo kwa nyadhifa tofauti, walikisababishia
hasara chuo hicho cha uhasibu kiasi cha Sh
6,258,448.60.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na
mwendesha mashitaka Kilongozi, washitakiwa
wote walikana mashitaka yao na hakimu wa
Mahakama hiyo, Mustapher Siyan alitoa
masharti ya dhamana ambayo ni kila
mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili
wafanyakazi wa serikali na kusaini bondi ya sh
milioni 1.
Hata hivyo washtakiwa hao wote walitimiza
masharti ya dhamana, huku hakimu akitoa
amri ya kukamatwa kwa washitakiwa wengine
watatu ambao ni Mwasaga, Melita na Malisa
ambao hawakufika mahakamani hapo.
Aliagiza popote walipo wakamatwe ili kufikia
Agosti Mosi wafike mahakamani hapo
kusomewa mashitaka yao.
Awali kabla ya kusoma kwa kesi hiyo ndani ya
chumba cha mahakama baadhi ya watumishi
kutoka chuoni hapo walitaka kuwadhibiti
waandishi wa habari ambao ni wapiga picha za
video wasifanye kazi zao, lakini wanahabari
walishinda kutokana na kuwa na kibali cha
kupiga picha mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews