Wednesday, October 7, 2015

Young Killer ajiunga na kundi la Mtu Chee, achukua nafasi ya Young Dee aliyejitoa

Baada kuwa kimya kwa takribani miaka miwili,
Kundi la Mtu Chee lililokuwa linaundwa na rappers
watatu, Ibrahim Mandingo a.k.a Country Boy,
David Genzi a.k.a Young Dee pamoja na
Boniventure Kabogo a.k.a Stamina linarudi rasmi
likiwa na mabadiliko.

Country Boy
Member na mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo
Country Boy amesema kuwa Mtu Chee imepata
member mpya ambaye ni Young Killer aliyechukua
nafasi ya Young Dee aliyejitoa kwenye kundi.

Akizungumzia sababu za Young Dee kujiondoa
Country Boy amesema “Kuna vitu ambavyo
vimeingiliana kutokana na kwamba Young Dee
amekuwa na majukumu yake na management
yake imekuwa kama inampa ugumu kufanya kazi
na sisi kwahiyo sisi tumeamua kuendeleza
kufanya, tumemuongeza Young Killer.” alsema
kupitia Planet Bongo ya EA Radio.

Ameongeza kuwa wanategemea kuachia wimbo
mpya wiki ijayo uitwao ‘Mimi’ ambao watakuwa
wamemshirikisha Jux na Vanessa Mdee.



Posted by 13

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews