Monday, October 12, 2015

Janet Jackson anaiandika historia tena kwa mara ya 7 na mauzo haya ya Album yake mpya!

Msanii wa muziki wa Pop nchini Marekani, Janet
Jackson anaziandika headlines kwenye stori za
burudani siku ya leo… Nimetembelea mtandao
wa Billboard na nimekutana na news kuhusiana
na Janet Jackson ambayo ningependa kushare
na wewe.

Je, unafahamu kuwa Janet Jackson ana jumla
ya Album 7 toka aanze kufanya muziki miaka ya
’80? na je unajua ni album zake ngapi
zimeshawahi kushika #1 moja kwenye chati ya
Billboard 200 ya Marekani ? kama hufahamu basi
ichukue hii…

Janet Jackson ameibuka kwenye nafasi ya
kwanza kwenye chati ya Billboard 200 na album
yake mpya kabisa ‘Unbreakable’ ambayo ni
album ya kwanza ya Janet baada ya kimya kingi
kwa muda wa miaka 7, sio hayo tu…
Billboard
imemtaja Janet Jackson kama msanii wa tatu
wa kike kuwa na Album 7 zilizoshika #1 ndani ya
miaka 40!
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard na Nielsen
Music , album mpya ya Janet Jackson ilitoka
tarehe 2 October 2015 na ndani ya wiki ya
kwanza tu album hiyo ilifanya mauzo ya juu
sana!
Hii ni audio Album ya kwanza ya Janet Jackson
toka Album yake ya mwaka 2008
‘Discpline’ ambayo pia kwa mujibu wa Billboard ,
Album hiyo iliibuka kwenye nafasi ya #1 kwenye
chati ya Billboard 200 … Album nyingine za Janet
Jackson zilizowahi kushika nafasi hiyo ni; All For
You (2001), The Velvet Rope (1997), Janet.
(1993), Janet Jackson’s Rhythm Nation 1814
(1989) na Control (1986).



Posted by 13

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews