Sunday, June 22, 2014
kauli ya uganda baada ya kuwekewa vikwazo na marekani kwa kupinga ushoga
Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa
Uganda, Balozi James Mugume, amesema
kuwa Uganda haitishwi na vikwazo
ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya
kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga.
Kwa mujibu wa BBC, Balozi Mugume
ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo
itafanya mazungumzo na Marekani ili
kufafanua hatua waliyochukua.
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria
hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na
maadili ambayo hayakubaliki katika jamii
nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo
havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na
pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii
kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko
la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
Labels:
flaviankachira
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment