Showing posts with label flaviankachira. Show all posts
Showing posts with label flaviankachira. Show all posts

Sunday, July 6, 2014

FIFA yalegeza adhabu ya suarez aruhusiwa kufanya mazoezi


FIFA imesema Luis Suarez ataruhusiwa
kufanya mazoezi na Liverpool wakati
akitumikia adhabu yake ya miezi minne na
mechi nane za kimataifa.

Wakati huohuo Uruguay imekata rufaa
kupinga adhabu hiyo.

Suarez alifungiwa
"shughuli zote zinazohusu kandanda" baada ya
kumng'ata Georgio Chiellini wa Italy.

Hata hivyo Claudio Sulser, mkuu wa kamati ya
nidhamu ya FIFA alipoulizwa siku ya Alhamisi
mjini Rio de Janeiro kuhusu adhabu hiyo
alisema:
Sulser pia amethibitisha kuwa Uruguay
imekata rufaa kupinga adhabu
iliyotolewa.

Claudio Sulser pia amesema Suarez
ambaye anasakwa na Barcelona,
ataruhusiwa kuhusika katika mchakato wa
uhamisho.

Saturday, June 28, 2014

Lulu: sina mda wakumbembeleza mwanaume coz wanaonitongaza kwa kwa siku ni wengi

Wakati wanawake wengine wakionekana kubembeleza penzi na kujinyenyekeza kwa wapenzi wao ili wasiachike, Lulu Michael anasema hana muda huo kwani uzuri wake unatosha kuwavuta wanaume wa kila aina kutoka katika kila kona ya Tanzania..... Lulu amedai kuwa inawezekana mwanaume wa kwanza kwake ndo chaguo lake namba moja, lakini suala la kuanza kulilia mapenzi au kuumia halipo na kamwe hawezi kufanya hivyo. "Mapenzi ni magumu hasa kwetu sisi wasanii. Kuna wanaume wanaweza kuja kwako ukadhani ni wema lakini baada ya kumaliza haja zao huwaoni, ndo maana huwa sioni haja ya kujilizaliza kwa mwanaume coz akigundua umezimika ndo kabisa atakugeuza Toilet paper ya kuchambia...... "Najua wapo wengi sana wanaonitamani, lakini kwa taarifa yao ni kwamba nipo makini sana na naitambua thamani yangu." Alisema Lulu. Hata hivyo Lulu alisema kuwa huwa anatongozwa na wanaume wengi sana kutokana na uzuri alionao, hali inayomfanya abadili namba ya simu kila mara kukwepa usumbufu.


Posted by flavian kachira

Thursday, June 26, 2014

Rick Ross auchoka unene,aamua kuingia gym

Rick Ross kila mtu anamjua kuwa na mwili mkubwa lakini hivi sasa ameamua kupugua kabisa. Mwenyewe anasema kwamba ameamua kujiweka fit na bado anakula anachokitaka lakini huwa anaenda gym kufanya mazoezi na ameshapunguza kilo 45.

Baada ya kumng'ata mchezaji suarez atolewa nje ya mashindano ya kombe la dunia

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng’ta mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil. Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya £65,680. Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.

zijue nyimbo 3 za kala jeremiah &Nay wa mitego ,Ben pol na Dyna zitakazotoka mwezi huu

R.kelly akwepa kujibu maswali juu ya kubadili njinsia kwa mtoto wake

Mwanamziki wa Marekani Robert Kelly maarufu kama R.kelly amekataa kujibu maswali yanayomhusu mtoto wake wa kike Jaya kubadilisha jinsia.kuwa wa kiume.R Kelly amekuwa akikwepa kujibu maswali hayo juu ya hatua ya mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 aliyotangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa amebadilisha jinsia yake na kuwa wa kiume akijiita Jay Kelly.Mwanamuziki huyo maarufu kutoka nchini Marekani amesema kuwa hatopenda kulizungumzia suala hilo la mtoto wake kujibadili jinsia na kuongeza kuwa hata kama kuna ukweli wowote hatovipa vyombo vya habari uhuru wa kuzungumzia.R Kelly ameongeza kuwa ni vyema watu wakaamini wanachokiona kwa macho kuliko wanachosikia kwani hata yeye amesikia juu ya suala hilo lakini si kweli.R Kelly amebarikiwa kuwa na watoto wengine wawili Joann Kelly na Junior Robert Kelly aliozaa na mke wake wazamani Andrea Kelly.

Hii ndo nguo atakayo vaa diamond kwenye tuzo za BET

BET Awards zinakaribia kufanyika na Diamond Platinumz anaelekea huko kwasababu amekuwa nominated kwenye kipengele cha Best African Act. Diamond atapita kwenye red carpet itakayo tumiwa na wasanii mbalimbali siku ya tukio. Hii ni sehemu ya nguo ambayo atavaa siku ya tukio na imetengenezwa na Sheria Ngowi, sehemu moja imeandikwa Mr Diamond Platnumz

Tarifaa ya kukanusha kufariki wa mbuge shukuru kawamba

Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza. UKWELI Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida. Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec) Mbunge -Chalinze

Sunday, June 22, 2014

kauli ya uganda baada ya kuwekewa vikwazo na marekani kwa kupinga ushoga

Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga. Kwa mujibu wa BBC, Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua. Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii nyingi za kiafrika. Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

Wema afunguka kwa uchungu baada ya watu kutoa lugha mbaya kwa mama yake

Wema Sepetu ameonekana kufungukia wale wanaomtukana kila siku na sasa kufikia hatua ya kumtukana hadi mama yake mzazi... Kupita mtandao mmoja wa kijamii, Picha moja ya mama mzazi wa Wema Sepetu iliyotengenezwa na kuwa CHAFU ilitolewa na kisha kuanza kushushiwa matusi mazito... Baada ya Picha na Matusi hayo, Wema amefunguka kwa uchungu kwa kuandika: "Dah...! Sijui hata niseme nini...! Ila si mlitaka kuniumiza... leo mmefanikiwa... nawapeni hongera.... Tena mmetisha haswa... Kila sjku huwa hata siumizwi na matusi yenu cuz naonaga kama ni mnajisumbua tu... Hakuna siku nimelia kwa uchungu kama leo... "I min mnitukane mimi mpaka mchoke but leave my mum out of it... Kawakosea nini nyinyi mama angu mpaka mfanye hivyo... Mzazi nwenyewe ndo nimebakia nae mmoja tu... mnataka afe na yeye nibaki yatima sio... dah... leo mmeniweza... saana jamani... Basi naomba isifike huko... nina uchungu sana na mama angu ... nampenda sana mama angu ila naona mnataka kuniulia mama angu... "Picha halisi ndo hio hapo juu kweli mtu uende ukamfanyie hivyo mama wa mwenzako... una mama wewe.. au uliokotwa na hujui uchungu wa mama... dah... nime surrender leo.... hongera zenu narudia tena... mmeniweza leo.... dah... "Mungu nipe nguvu ktk hili jamani... Kwani nilichokikosea haswa ni kitu gani mpaka iwe hivi . Nimekosa nini mimi yarabi toba.... Eeeh mungu... Dah... Ila nashkuru..." Ameandika Wema Sepetu kwa Uchungu

Total Pageviews