
FIFA imesema Luis Suarez ataruhusiwa
kufanya mazoezi na Liverpool wakati
akitumikia adhabu yake ya miezi minne na
mechi nane za kimataifa.
Wakati huohuo Uruguay imekata rufaa
kupinga adhabu hiyo.
Suarez alifungiwa
"shughuli zote zinazohusu kandanda" baada ya
kumng'ata Georgio Chiellini wa Italy.
Hata hivyo Claudio Sulser, mkuu wa kamati ya
nidhamu ya FIFA alipoulizwa siku ya Alhamisi
mjini Rio de Janeiro kuhusu adhabu hiyo
alisema:
Sulser pia amethibitisha kuwa Uruguay
imekata rufaa kupinga adhabu
iliyotolewa.
Claudio Sulser pia amesema Suarez
ambaye anasakwa na Barcelona,
ataruhusiwa kuhusika katika mchakato wa
uhamisho.
No comments:
Post a Comment