
Baada ya uwepo wa tetesi za kuihama
Liverpool kushika hatamu kwa takribani wiki 3
sasa, hatimaye leo hii Luis Suarez amejiunga
rasmi na FC Barcelona akitokea Liverpool.
Usajili wa Suarez umeigharimu FC Barcelona
kiasi cha £65m kwa mujibu wa mtandao wa
Barcelona, na hii ni rekodi kwa Liverpool –
Suarez anakuwa mchezaji aliyeuzwa kwa fedha
nyingi zaidi na klabu hiyo iliyoshika nafasi ya
pili kwenye EPL msimu uliopita.
Suarez ambaye alijiunga na Liverpool akitokea
Ajax, pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji
anayeshika nafasi ya nne kwa kusajiliwa kwa
fedha nyingi zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na
Neymar.
Hata hivyo pamoja na usajili huo mchezaji
huyo hatoweza kuitumikia Barca mpaka
adhabu yake ya kufungiwa mechi 8 na kifungo
cha miezi 4 kitakapoisha.

No comments:
Post a Comment