
Diamond Platinumz alipokewa kwa shangwe
jana (July 10) katika uwanja wa kimataifa wa
Julius Nyerere na wadau mbalimbali wa muziki
na mashabiki wake akitokea Marekani
alikoenda kushiriki katika tuzo za BET.
Wema Abraham Sepetu alifika pia katika
uwanja huo kumpokea asali wake wa Moyo na
alipata nafasi ya kuzungumza na Fadhili Haule,
mtangazaji wa kipindi cha Sunrise cha 100.5
Times Fm aliyetaka kupata maoni yake kuhusu
video mbili mpya za Diamond zilizotoka hivi
karibuni ‘MdogoMdogo na Bum Bum
aliyomshirikisha Iyanya’.
Wema alifunguka huku akiweka akilini kuwa
anamzungumzia asali wake wa moyo hivyo
lugha na points zote alizitumia vyema.
“Well, honestly nimeipokea vizuri.
Kitu
chochote anachokifanya mpenzi lazima
utakiona kizuri hata kama ni kafanya kibaya
utakiona kizuri tu. Kwa hiyo amejitahidi, he is
on another level na huwezi kumfananisha na
msanii yoyote Tanzania na haangushi
mashabiki wake. Unachokitegemea anafanya
zaidi” Amesema.
Ameeleza kuwa kwenye video ya MdogoMdogo
alifanya kitu tofauti na watu walichokuwa
wanategemea kwa jinsi wanavyomfahamu
Diamond na mitindo yake.
“Watu walikuwa wanategemea kuwa video
itakuwa…labda ataenda uswahilini sijui nini,
lakini yeye kaifanya very international and
nimeipenda the fact kwamba kuna
uinternational lakini pia kuna uafrika ndani
yake, so it’s nice.”
“Bum Bum, it’s nice. Like Bum Bum imeenda
sana International like soko la nje sanasana.
Na ndio maana hamjaona akirelease audio
yake.
And the video…yaani everything is nice,
siwezi kum-criticize baby wangu.” Ameeleza
Wema Sepetu.
Katika hatua nyingine, Wema ambaye ameahidi
kuwa pamoja na Diamond katika yote
amesema tayari ameshazungumza nae kuhusu
hatua aliyoifanya ya kumkutanisha na waigizaji
wa kimataifa na mashabiki wao wakae mkao
wa kupokea kitu kikubwa katika tasnia ya
filamu.
No comments:
Post a Comment