Friday, February 6, 2015

Shindalo la Tutoke na Serengeti limebakiza wiki tatu .....Kazi kwako mdau, bado hujachelewa

Dar es Salaam, Tanzania: 04th Februari, 2015.
Kampuni ya pili kwa ukubwa katika utengenezaji
wa pombe hapa nchini imeeleza kwamba
kampeni yake inayoendelea ya “Tutoke na
Serengeti” inaelekea ukingoni.
Kwa kigezo hicho, kampuni hiyo imejipanga
kumaliza kampeni hiyo kwa kishindo na njia ya
kipekee kwa kuhakikisha kwamba washindi
wengi zaidi wanapata nafasi ya kujishindia
zawadi mbalimbali ambazo ziliorodheshwa hapo
mwanzo.

Akiongea na waandishi wa habari ndani ya
makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo
Chang’ombe-Dar es salaam, Meneja Chapa wa
bia ya Serengeti Premium Bw. Rugambo Rodney
alizitaja baadhi ya zawadi ambazo zinasubiri
washindi wengi zaidi kuzinyakua kama;- Limo
Bajaj, safari ya kutembelea mbuga za wanyama
ijulikanayo kama “Mtoko wa mbugani”, fedha za
papo kwa hapo, bia za bure ambazo
zinapatikana katika maeneo yote ya mauzo nchi
nzima pamoja na bia za punguzo.

“Ninafurahi kuona kwamba promosheni hii
imepeta mwitikio mzuri Tanzania nzima na
kama kampuni tunajivunia kwa kuweza kutoa
zawadi mbalimbali kwa wateja wetu kama
shukrani kwa kuwa pamoja na sisi….
Ninachoshukuru zaidi ni kwamba zawadi nyingi
tulizotoa zimeweza kuongeza vipato kwenye
maisha ya washindi wetu... Bado naamini kuna
watanzania wengi ambao wanatamani
kutembelea mbuga za wanyama, kumiliki Limo
Bajaj au hata kujishindia fedha taslimu.”
Rodney aliongeza kwamba muda bado bado upo
na wakati ndio huu, ingawa zimebaki wiki tatu tu
kwa wateja kujikusanyia zawadi hizo.
Aliendelea kuwakumbusha wateja kwamba,
kushinda zawadi hizi ni rahisi sana.
Unachotakiwa kufanya ni kununua kinywaji cha
Serengeti Premium Lager, ambacho ndio kinywaji
rasmi kinachodhamini kampeni hiyo na mteja
aangalie chini ya kizibo ambako atakuta namba
ambazo zinatakiwa kutumwa kwa njia ya SMS
katika namba 15317 na moja kwa moja atakuwa
ameingizwa katika droo na kuwa katika nafasi
ya kujinyakulia zawadi hizo.

SBL pia ilithibitisha mbele ya waandishi wa
habari kwamba tayari imeshakabidhi Limo Bajaj
tano kwa washindi mbalimbali, wawili kutika
mkoa wa Kilimanjaro, mmoja kutoka mkoa wa
Morogoro na wawili wengine kutoka mkoa wa
Dar es Salaam.

Pia wengi wamejishindia safari za kutembelea
mbuga ya wanyama ya Serengeti kwa watu
waili, Fedha taslimu Tshs. 100,000
zimeshatolewa kwa washindi zaidi ya 15 kila
wiki na bia za bure kwa washindi mbalimbali
katika kipindi chote hiki cha kampeni.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews