Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria zinasema kuwa zaidi ya wanawake 60
wakiwemo wasichana wa umri mdogo
waliotekwa nyara mwezi jana na Boko Haram
wamekwepa.
Taarifa hii inakuja wakati sawa na taarifa za
kutokea makabiliano makali kati ya jeshi la
Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni
mwa wanawake 68 waliotekwa nyara mwezi
uliopita karibu na mji wa Damboa Kaskazni
Mashariki mwa jimbo la Borno.
Serikali ya Nigeria imeitisha uchunguzi wa kina
juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
Hali ya usama ani mbaya sana huku miundo
mbinu duni ikichangia kuifanya hali ngumu
kuweza kufikia maficho ya kundi hilo na pia
kubaini idadi ya wasichana waliotoroka kutoka
mikononi mwa Boko Haram.
BBC imeongea na jamaa ya wasichana watatu
ambao walitoroka. Sasa wako salama
nyumbani kwao na mmoja wao amesema
kwamba wasichana wengi wamefanikiwa
kutoroka.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo
vinadai kuwa huenda wasichana hao
walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara
walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi.
Maafisa wakuu hata hivyo bado hawajaweza
kuthibitisha kukwepa kwa wasichana hao.
Wakati huohuo hapajakuwa na taarifa zozote
kuhusu wasichana 200 waliotekwa nyara katika
shule ye mabweni ya Chibok mwezi Aprili.
Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya
kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile
Marekani, Uingereza na hata Ufaransa
wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria
kuwasaka wasichana hao.

No comments:
Post a Comment