Uhusiano kati ya Davido na Diamond Platnumz
ulishavunjika siku nyingi kufuatia issue iliyotokea
mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big
Brother Africa.
Davido na Diamond Platnumz akiwa studio
mwishoni mwa mwaka juzi
Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa
tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini
kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi
kumshirikisha kwenye remix ya Number One
iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka
katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi
kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa
‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu
wimbo mpya Davido kwenye Instagram.
Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado
ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye
ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao
wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa
baadaye.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido
amepost picha ya zamani akiwa na Diamond
kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha
hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a
sweeter love song than AYE .. Hmm this album
yo.”
Picha hiyo imevutia comments nyingi japo
asilimia kubwa ni za wakenya wanaomnyeshea
mvua ya matusi! Yes, Wakenya hawataki
kumsikia tena Davido!
Hakuna shaka kuwa staa huyo wa Nigeria ana
picha nyingi ambazo angeweka kuambatanisha na
ujumbe huo. Hivyo, uchaguzi wa picha akiwa na
Diamond unaweza ukawa na dhumuni maalum!
No comments:
Post a Comment