Friday, July 4, 2014

Atupwa jela kwa kumuvunja mke mguu

Mkazi wa Kijiji cha Nyasoro wilayani Rorya
mkoani Mara, Ernest Zabron (60)
amehukumiwa kwenda jela miezi sita kwa kosa
la kumpiga mkewe Esther Ernest (42) kwa
rungu na kumvunja mguu wake wa kushoto.

Hata hivyo, Zabron katika utetezi wake
hakuonesha kujutia kumshambulia mkewe na
kumvunja mguu.
Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 537/2011
ilisomwa Juni 30 mwaka huu na Hakimu wa
Mahakama ya Wilaya Tarime, Odira Amworo.

Awali mwendesha mashitaka wa Polisi, Abel
Kazen alidai mbele ya hakimu kuwa Zabron
alimshambulia mkewe katika ugomvi wao
uliotokea Saa 2:00 usiku wa Desemba 7
mwaka 2011 nyumbani kwao katika Kijiji cha
Nyasoro.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi
wawili na PF3 inayoonesha kuvunjika mguu
wa kushoto wa Esther kutokana na kipigo.

Ernest, mbali na kukana mashitaka mahakama
ilidai kuwa hakuonesha kujutia kitendo
alichofanya cha kumshambulia mzazi
mwenzake na kumvunja mguu na
kumsababishia ulemavu.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Odira alisema,
"kutokana na kuonesha ukorofi na kutojutia
kitendo ulichomfanyia mzazi mwenzako na
kuhukumu kwenda jela miezi sita bila faini ili
iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama
hizo".

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews