Showing posts with label flavian kachira. Show all posts
Showing posts with label flavian kachira. Show all posts

Monday, July 7, 2014

Rachel nae alishwa UNGA (MADAWA YA KULEVYA)

Kama ilivyotokea kwa msanii nyota wa
kike wa bongo fleva, Rehema Chalamira
'Ray C' kuingizwa katika matumizi ya dawa
ya kulevya na mtu ambaye alitokea
kumwamini sana, ndivyo ilivyotokea sasa
kwa msanii anayefuata nyendo zake,
Winfrida Josephat 'Rachel' ambapo
anadaiwa kuvutishwa unga bila kujua....
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha karibu
na msanii huyo,Rachel amewekewa dawa
hizo kupitia kwenye bangi na wakati
mwingine kwenye sigara hivyo inakuwa
vigumu kubaini hila iliyofanyika....
Habari ambazo tumezipata zinadai kwamba
msanii wa kiume nyota wa bongo fleva
ambaye amewahi kutuhumiwa kutumia
dawa za kulevya ndiye anayemtengenezea
kokuteli hiyo inayotarajiwa kumwangamiza
siku za usoni....
"Huyu mtoto ameshaanza kutumia dawa
za kulevya.Huwezi amini, hata Ray C
ameshapewa taarifa, hivyo anamsaka
kuhakikisha anamtoa katika kifungo
alichojiingiza...
"Unajua Ray C anampenda sana kutokana
na namna anavyopenda kujiweka kama
yeye na hata jinsi anavyoimba nyimbo
zake, hivyo aliposikia madai hayo alianza
kumsaka kila kona lakini bado
hajafanikiwa kwani Rachel anamkimbia,"
kimesema chanzo hicho.
Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa
kutokana na namna Rachel anavyomuamini
msanii huyo wa kiume hajakubali kama
anachanganyiwa dawa za kulevya kwenye
bangi na sigara.
"Mwenyewe anajiona yupo sawa, lakini sisi
tunaona tofauti, hakika Rachel anapotea na
sijui nani atamuokoa.
"Tumeshamwabia kwamba anapotea lakini
haamini, tunaweza kusema kwamba Ray C
aliponea bahati, sasa sijui kama na yeye
atapata bahati kama alivyopata mwenzake,
" kilisema chanzo hicho
Rachel ambaye anatamba na wimbo wa
'upepo' hakuweza kupatikana kuzungumzia
tuhuma hizo

wananchi wafurahia Raisi kujumuika nao katika maonyesho ya saba saba


Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai
6, 2014 alitembelea kwa mara ya pili
maonesho ya kimataifa ya bishara katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya
Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake
kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya siku
ya Jumamosi kutokana na muda.

Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa
naye karibu kama ambavyo yeye pia alifurahi
kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila
mwaka.

Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais
Kikwete ambapo kila mara alisimama na
kuwasalimia.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na
baadhi ya wananchi waliotembelea maonyesho
ya Sabasaba.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta na watoto
aliokutana nao Sabasaba.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaaga wananchi
mara baada ya kujumuika nao pamoja kwenye
Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar.




Baby madah aenda kwao kutambika baada yakuona mambo hayaendi vizuri

Staa wa filamu na muziki Bongo, Baby
Madaha anadaiwa kwenda kijijini kwao
kutambika baada ya kuona mambo yake
yanamwendea kombo.
Akizungumza na mwanahabari wetu, rafiki wa
karibu wa Baby Madaha ambaye hakupenda
kuanikwa, alisema kutokana na staa huyo
kuona mambo hayaendi vizuri hasa kwenye
muziki, ameamua kwenda nyumbani kwao
Mwanza kwa ajili ya kutambikia mizimu ya
kwao.

Alipotafutwa Baby kuhusiana na ishu hiyo,
alifunguka:
“Ni kweli niko nyumbani kwetu Mwanza, ni
muda mrefu sijaja kumuona mama, kuhusu
kutambika hilo ni lazima kwani nikiona
mambo hayaendi vizuri, lazima niikumbuke
mizimu ya kwetu,” alisema Baby.

Angalia mapenzi ya shabiki huyu mdogo kwa mchezaji Neymar


Ukizungumzia taifa ambalo limetoa mastar
kadhaa wa soka Duniani hutoacha kulitaja
Brazil hii ni kufuatia rekodi zake kadhaa
ambazo limewahi kujiwekea kwenye medali ya
soka duniani leo limeingia kwa headline tena
taifa hili.

Ni kuhusu mtoto mdogo amabye kwa
kumtazama anaweza kuwa na umri usiozidi
miaka 3,amekua ni miongoni kati ya
walioumizwa na taarifa za kidaktari
zinazomhusu mchezaji Neymar kuwa
hatocheza mechi nyingine za Kombe la Dunia.

Kama unakumbuka Neymar alipata majeraha
baada ya kuumia kwenye mechi iliyochezwa
kati ya Brazil na Colombia na katika mechi
hiyo Brazil ilifanikiwa kushinda goli 2-1 na
kufanikiwa kuingia nusu Fainali.
July 08 Brazil ambao kimsingi ndio wenyeji wa
mashindano haya ya kombe la dunia itacheza
na Ujeruman,mchezo utakaochezwa bila
Neymar katika mechi ya Nusu Fainali.

Picha za mchezaji Neymar akisafilishwa na helcopter akitoka hospital

Mchezaji aliyekuwa tegemezi kwenye mechi za
kombe la dunia za timu ya Brazil Neymar Jr,
hatimaye amepelekwa kwao Guaruya, Sao
Paulo kwa ajili ya mapumziko. Neymar
amepata matibabu baada ya kupata maumivu
kwa kugongwa kifuti kwenye uti wa mgongo
na mchezaji wa Colombia wakiwa uwanjani.
Neymar alipelekwa na helicopter kwenye
uwanja wa mazoezi ambapo alikutana na
wachezaji wenzake, baadae alikutana na
waandishi pamoja na mashabiki na safari
ikaelekea Sao Paulo.










Sunday, July 6, 2014

Dayna nyange AMTEGA tena diamond platnumz

Mwanamuziki anayefanya vizuri katika
gemu Dayna Nyange amesambaza beat ya
wimbo wake mpya ambao tayari
ameshaurekodi kwa lengo la kuwapima
wasanii wezi wa beats za wenzao kama
wataufanyizia tena.....

Hatua ya Dayna imekuja kutokana na
malalamiko aliyowahi kuyatoa siku za
nyuma ya kuibiwa beat ya wimbo wa
Number One na msanii Diamond Plutnumz
baada ya kumsikilizisha beat hiyo na
kumtaka afanye naye collabo.....

"Safari hii nimeacha akili yangu na hisia
zangu zitawale katika kile ambacho nina
kiamini kuwa ni sahihi kwangu hasa
katika huu wimbo mpya, tayari
nimeurekodi lakini nimewasambazia beat ili
nione nani atakayethubutu kuiba kama
ilivyokuwa mwaka jana," alisema Dayna
ambaye hivi sasa inasemekana yupo
kimapenzi na mshiriki wa big brother,
Nando.

Licha ya Dayna kutomtaja Diamond moja
kwa moja katika mtego wake huo lakini
ukweli unabaki palepale kwamba aliwahi
kumshutumu mwanamuziki huyo pamoja
na prodyuza Sheddy Clever kwa wizi wa
beat na kesi yao ilifika hadi Basata na
Cosota

Hiki ndicho kikubwa atakacho fanya diamond siku ya birthday ya mama yake mzazi

Mama yake Diamond amezaliwa tarehe 7/7 na
siku hiyo Diamond amepanga kufanya kitu
kikubwa akiwa anasherekea.

Mwaka huu
anafanya kitu ambacho hadi mashabiki zake
watafurahia siku hiyo na hii ni nafasi yako
kukijua.


Kilichojiri kwenye mechi ya uholanzi Vs costa rica -

Historia mpya imeandikwa kwenye mechi ya
mwisho ya hatua ya nane bora iliyozikutanisha
Uholanzi dhidi ya timu ya Costa Rica, ambayo
kwa mara ya kwanza imefanikiwa kucheza
hatua ya robo fainali ya kombe la dunia.

Mchezo huo uliomalizika hivi punde umetumia
zaidi ya dakika 120 ili kuamua timu ya kwenda
kuchuana na Argentina kwenye nusu fainali.

Dakika 90 za mchezo huo ziliisha kwa
matokeo ya sare tasa, na mpaka mpira
unakwenda dakika 30 za nyongeza na
kumalizika milango bado ikabaki migumu na
ikaamuliwa kwenda kwenye mikwaju ya penati.

Uholanzi ikiwa haijawahi kushinda kwenye
mikwaju ya penati katika mashindano ya
kombe la dunia, ikafanikiwa kushinda kwa
penati 4-2 dhidi ya Costa Rica.

Pia hii ni mara ya kwanza kwa Uholanzi
kushinda mechi yoyote ambayo imevuka
kwenda kwenye hatua ya dakika za nyongeza.

Kwa matokeo hayo sasa Argentina itakutana
na Holland jumatano usiku, wakati Brazil
ikukutana na Ujerumani jumatatu hii.

Saturday, July 5, 2014

Msichana wa uingereza ashiriki vitendo vya ngono na wanaume 24 hadharan iliajishindie zawadi

Kiu ya kushinda zawadi yenye jina
lililomsafirisha kimawazo imemponza
msichana mmoja Muingereza baada ya
kuamua kutoa utu wake na kukubali kushiriki
kwenye mchezo wa kufanya vitendo vya ngono
(bl*w*job) na wanaume 24 hadharani kwenye
club ya usiku ili ashinde ‘Holiday’.

‘Holiday’ ni jina la kinywaji cha cocktail
kilichotengenezwa na gin, vodka, peach
schnapps, blackcurrant liqueur na fruit juice.

Lakini masikini msichana huyo mwenye miaka
18 hakulifahamu hilo, ndio maana alijitoa
muhanga kushiriki katika mchezo huo
uliofanyika kwenye bar iitwayo Alex’s Bar
huko Hispania.

Binti huyo ambaye jina limehifadhiwa
aliambiwa na waandaaji wa mchezo huo kuwa
endapo atashiriki basi atajishindia ‘Holiday’,
lakini mwisho wa siku kumbe zawadi ni ya
kinywaji cha cocktail kinachogharimu £4 sawa
na elfu 11 ya kibongo.

Msichana huyo alikuwa akishangiliwa na umati
uliokuwa ukishuhudia mchezo huo mchafu
huku wengine wakirekodi tukio hilo kwenye
simu zao.

“Msichana huyo alikuwa akihamasishwa
kunywa sana na kuambiwa atashinda ‘holiday’
kama atashiriki kwenye mchezo huo.

Kwabahati mbaya ‘Holiday’ hiyo ikageuka kuwa ni
jina la kinywaji cha cocktail. Namwonea
huruma” shuhuda mmoja aliiambia gazeti la
The Sun.

Mtoto aliezaliwa na miguu mitatu

Mtoto mdogo ambaye amezaliwa na miguu
mitatu amesafirishwa kwenda nchini Marekani
kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kuondoa
miguu miwili
Ana Paula mwenye miezi 22 alikuwa ni pacha
aliyeungana ambapo dada yake hakuweza
kupona wakati wa upasuaji wa
kuwatenganisha.
Ni mguu mmoja tu wa mtoto huyo unaofanya
kazi hivyo upasuaji atakaofanyiwa katika moja
ya hospitali za watoto ni kuondoa miguu
miwili ambayo haifanyi kazi na kumwongezea
uwezo wa viungo vyake kufanya kazi.
Ana na mama yake walisafirishwa kutoka
Panama kwa msaada waliopatiwa na
wasamaria ili zoezi zima liweze kukamilika.




Nigeria kufungiwa soka na FIFA kwa sababu hii

Baada ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora
ya kombe la dunia mabingwa wa Afrika
Nigeria wapo hatarini kukumbwa na balaa
lingine.

Mabingwa hao wa Afrika huenda wakapigwa
marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya
soka baada ya mahakama nchini humo
kutengua utawala wote ya shirikisho la soka
nchini humo
Waziri wa michezo wa Nigeria Tammy
Danagogo alimteua Lawrence Katiken kuwa
msimamizi mkuu wa NFF.

Taarifa nchini humo zinasema kuwa matokeo
duni ya timu hiyo hayakusaidia hali mbaya ya
uhusiano na serikali ya nchi hiyo na shirikisho
la soka.

Super Eagles iliambulia kichapo cha 2-0
mikononi mwa Ufaransa katika raundi ya pili
ya kombe la dunia na hivyo kufungashwa
virago.

Mahakama ya jimbo la Plateau ilitoa amri ya
kupinga uongozi wa Aminu Maigari, na kamati
yake nzima.

Kufuatia hatua hiyo Nigeria inaweza
kuadhibiwa na FIFA ambayo inakataza
mamlaka za kiserikali kuingilia mambo ya
soka.

Tanzania yapaa kijeshi.....JWTZ yatajwa kuwa katika vikosi bora 35 dunian vilivyoandaliwa kwa oparesheni za kijeshi

Majeshi Maalum (Special Forces) ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35
vya majeshi ya nchi mbali duniani
vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu,
uwezo mkubwa wa kupigana na
vilivyofundishwa vizuri.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via
Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi
pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake
miongoni mwa majeshi bora duniani.

Chini ya kichwa cha habari “35 Most Badass
Elite Fighting Units from Around the
World” mwandishi, Micky Wren anaandika
kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani,
yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa,
yana silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa
vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi
na yenye uwezo kukabiliana na adui katika
mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni wa
utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye
uwezo mkubwa.
Mwandishi anasema kuwa orodha hiyo
haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa
kijeshi wa kila kikundi.

Vikosi vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile
cha Seal cha Jeshi la Maji la Marekani, SAS cha
Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha
Majeshi Maalum ya Denmark, Majeshi Maalum
ya Ufaransa, Kikosi cha MARSOC, Majeshi
Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za
usoni zisizoweza kuingiliwa na risasi na Kikosi
cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya
Ireland.
Vingine ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi
Maalum cha Kukabiliana na Ugaidi cha JTF2
cha Canada, Majeshi Maalum ya Uholanzi,
Kikosi cha SBS, Majeshi Maalum ya Jamhuri ya
Korea, Majeshi Maalum ya Ufaransa, Majeshi
Maalum ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha
Norway, Canadian Joint Response Unit cha
Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi
cha French Commando Marine, Majeshi
Maalum ya New Zealand, Kikosi cha
Norwegian Armed Forces Special Command na
Kikosi cha Polish Grom cha Poland.
Vingine ni Kikosi cha US Army Special Forces
Sniper with Remington Modular Sniper Rifle,
Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi Maalum
ya Indonesia, Majeshi Maalum ya Romania,
Kikosi cha SASR cha Australia, Kikosi cha KSK
cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani,
Majeshi Maalum ya Israel – Shayetet 13,
Majeshi Maalum ya Urusi – Spetsnaz, Majeshi
Maalum ya Austria – Jagdkommando, Majeshi
Maalum ya Iraq, Majeshi Maalum ya
Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya
Peru.

Dudu Baya anasakwa na polisi

MKONGWE wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini
‘Dudubaya’ anasakwa na polisi kwa RB namba
OB/RB/11650/2014 KUTISHIA KUUA mganga
wa jadi Mery Kapalisya ambaye inadaiwa
alikuwa akiishi naye kama mkewe.

Akisimulia mkasa mzima, Mery alisema
Dudubaya alitishia kumuua mara baada ya
kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi
pamoja maeneo ya Tandale, jijini Dar.

“Mimi na Dudu (Dudubaya) tulikutana baada
ya kukutanishwa na Mabovu (msanii) ndipo
tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi baada ya
kuniomba niwe naye na kunieleza matatizo
yake.

“Kwa sababu nilimpenda niliamua kumkubalia
na kuanza naye maisha ambapo tulikuwa
tukilala katika baa yangu nyumbani kwa akina
Mabovu.

“Tukiwa ndani ya uhusiano, Dudubaya alianza
kunibembeleza kwamba baa ile tuipe jina la
Mamba ikiwa ni chata yake, kwa sababu
nilimpenda niliamua kumkubalia lakini
nilimwambia aongeze herufi nyingine mbili
ambazo zitamaanisha na mimi nahusika,
tukakubaliana,” alisema Mery na kuongeza:

“Baada ya baa kubadilishwa jina, matatizo
yakaanza taratibu kwani walijaa wasanii wa
kila aina, baa ikaanza kuwa na sifa mbaya
mpaka wateja wote wakaondoka wale
waliokuwa wanajiheshimu.

Mery alisema alikuwa akimuonya Dudubaya
juu ya tabia za kumsaliti na kulala na
wanawake ndani ya nyumba pale anapokuwa
amesafiri kwenda kwenye mambo ya kitabibu
lakini alikuwa hasikii.

“Baada ya kunifukuza nyumbani, amenitumia
maneno mazito sana ambayo siwezi kusimulia
kiukweli lakini ninao ushahidi wa SMS,”
alisema Mery alipokuwa katika Kituo cha Polisi
Oysterbay.

Wakati Mery alipokuwa kituoni hapo, polisi
walimpigia simu Dudubaya, akasikiliza maelezo
ya polisi kisha akakata simu na alipopigiwa
tena, hakupokea.


Friday, July 4, 2014

Wema sepetu aomba msadaa TCRA kumsaka mtu alie tengeneza picha chafu ya mama yake mzazi

Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu
ameiomba Wizara ya Sayansi na Teknolojia
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
( TCRA ) kumsaka mtu aliyetengeneza
picha chafu ya mama yake mzazi,
Mariam Sepetu na kisha kuisambaza
kwenye mitandao ya kijamii......

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema
alisema anaamini kuwa TCRA wanao
uwezo wa kumbaini mtu huyo ambaye
bado hajamfahamu ili sheria iweze
kuchukua mkondo wake kwani
amemdhalilisha mzazi wake bila sababu
yoyote....

"Nafanya utaratibu wa kwenda TCRA ili
wamsake aliyefanya kitendo hicho kwani
uwezo huo wanao,"

alisema Wema
Mrembo huyo alisema serikali isisubiri
mpaka tukio hilo limkute kiongozi wa
serikali ndo waanze kuhaha kwani tabia
hiyo inaonekana kuota mizizi baada ya
hivi karibuni kufanyiwa hivyo wabunge.


Wasanii dude na tino watiwa mbaroni siku nzima nchini kenya

Muigizaji nguli wa filamu za kibongo
nchini Kulwa Kikumba 'Dude' amesema
askari wa Kenya waliwakamata na
kuwashikiria kwa siku nzima wakiwa
wanarekodi movie yao mpya yeye na
wasanii wenzake ambao ni mzee Majuto
na Tino maeneo ya Maduka Kifili mjini
Mombasa.....
"Nchi ya Kenya kwa sasa ina ulinzi mkali
sana, askari wapo kila kona, tulikamatwa
kwa muda mrefu sana wakidhani ni
waharifu.

"Ilitupoteza sana muda. Pamoja na
kuwaonyesha Passport na vitambulisho
vyetu, askari wale hawakutuelewa mpaka
watu wa shirikisho la Filamu pale
Mombaa walipokuja kutusaidia," alisema
Dude

Wizara ya Afya ya waonya madaktari feki

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini
Tanzania imewaonya watu wanaojiita
madaktari na maprofesa bila ya kuwa na sifa
hizo huku wakidai kuwa na uwezo wa kutibu
magonjwa yasiyotibika ukiwemo ugonjwa wa
Ukimwi na kisukari.

Mganga mkuu wa serikali Dkt Donnan
Mmbando ametoa onyo hilo jijini Dar es
Salaam jana, na kufafanua kuwa wenye haki ya
kujiita hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni
zinazosimamia tiba asili na tiba mbadala
nchini Tanzania, ni wale tu wenye sifa
zinazotambulika na mamlaka mbalimbali za
serikali.

Dkt Mmbando amesema inashangaza kuona
watu wakijitangaza na kujinadi eti ni
madaktari na wana uwezo wa kutibu
magonjwa hayo na mengine ambayo
yameshindikana ilhali sio kweli bali ni njia za
kijanja za kutaka kujipatia pesa.

Aidha, Dkt Mmbando amesema katika
kuhakikisha dawa za tiba asili na tiba mbadala
zinatolewa kwa mujibu wa viwango
vinavyotambulika kisheria, wizara inakamilisha
taratibu kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda
kitakachokuwa na jukumu la kusindika dawa
zote za asili ili ziwe katika mwonekano na
viwango vya kisasa.

Usindikaji huo kwa mujibu wa Dkt Mmbando,
utafanana na dawa zinazotumiwa katika
hospitali na vituo vya huduma za kisasa, hatua
itakayowafanya wananchi waachane na
kuchemsha mizizi na kunywa katika hali
ambayo hairidhishi kiafya.

Atupwa jela kwa kumuvunja mke mguu

Mkazi wa Kijiji cha Nyasoro wilayani Rorya
mkoani Mara, Ernest Zabron (60)
amehukumiwa kwenda jela miezi sita kwa kosa
la kumpiga mkewe Esther Ernest (42) kwa
rungu na kumvunja mguu wake wa kushoto.

Hata hivyo, Zabron katika utetezi wake
hakuonesha kujutia kumshambulia mkewe na
kumvunja mguu.
Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 537/2011
ilisomwa Juni 30 mwaka huu na Hakimu wa
Mahakama ya Wilaya Tarime, Odira Amworo.

Awali mwendesha mashitaka wa Polisi, Abel
Kazen alidai mbele ya hakimu kuwa Zabron
alimshambulia mkewe katika ugomvi wao
uliotokea Saa 2:00 usiku wa Desemba 7
mwaka 2011 nyumbani kwao katika Kijiji cha
Nyasoro.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi
wawili na PF3 inayoonesha kuvunjika mguu
wa kushoto wa Esther kutokana na kipigo.

Ernest, mbali na kukana mashitaka mahakama
ilidai kuwa hakuonesha kujutia kitendo
alichofanya cha kumshambulia mzazi
mwenzake na kumvunja mguu na
kumsababishia ulemavu.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Odira alisema,
"kutokana na kuonesha ukorofi na kutojutia
kitendo ulichomfanyia mzazi mwenzako na
kuhukumu kwenda jela miezi sita bila faini ili
iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama
hizo".

Mwili wa kaimu balozi wa libya wasafirishwa kurudi kwao

Mwili wa Kaimu Balozi wa Libya nchini, Ismail
Nwairat (39), umesafirishwa jana kwenda Libya
na shirika la ndege ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Ofisi ya
Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, mwili wa balozi
huyo anayedaiwa kujiua kwa risasi Jumanne
wiki hii mchana akiwa ofisini kwake, mwili
wake utapokewa na ndugu zake.

Na kwamba taarifa zaidi juu ya maziko ya
balozi huyo zitatolewa na ndugu zake baada
kuupokea mwili huo nchini Libya.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar
es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi
wa kifo cha kaimu balozi huyo umeanza na
kwamba watachunguza sababu za kujiua.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano cha wizara hiyo, Mkumbwa Ally,
tukio hilo limeshtua Tanzania kwa kuwa si
jambo la kawaida kwa mwanadiplomasia
kujiua..

Total Pageviews