Saturday, July 5, 2014

Nigeria kufungiwa soka na FIFA kwa sababu hii

Baada ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora
ya kombe la dunia mabingwa wa Afrika
Nigeria wapo hatarini kukumbwa na balaa
lingine.

Mabingwa hao wa Afrika huenda wakapigwa
marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya
soka baada ya mahakama nchini humo
kutengua utawala wote ya shirikisho la soka
nchini humo
Waziri wa michezo wa Nigeria Tammy
Danagogo alimteua Lawrence Katiken kuwa
msimamizi mkuu wa NFF.

Taarifa nchini humo zinasema kuwa matokeo
duni ya timu hiyo hayakusaidia hali mbaya ya
uhusiano na serikali ya nchi hiyo na shirikisho
la soka.

Super Eagles iliambulia kichapo cha 2-0
mikononi mwa Ufaransa katika raundi ya pili
ya kombe la dunia na hivyo kufungashwa
virago.

Mahakama ya jimbo la Plateau ilitoa amri ya
kupinga uongozi wa Aminu Maigari, na kamati
yake nzima.

Kufuatia hatua hiyo Nigeria inaweza
kuadhibiwa na FIFA ambayo inakataza
mamlaka za kiserikali kuingilia mambo ya
soka.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews